1. Vigezo na Masharti:
i)    Huduma hii ni kwa ajili ajili wa wateja wa Tigo wa malipo ya awali.
ii)    Kampeni hii itafanyika kwa muda wa Miezi 3 tu.
iii)    Tarehe ya kumalizika kwa kampeni inaweza kubadilika kwa kutegemea muenendo wa utoaji wa Zawadi.
iv)    Kila mteja anayeshiriki kampeni hii kwa washindi wa siku na wiki wananafasi sawa ya kushinda kwa kua mshindi atachaguliwa kwa kufanya DROO, na kwa MSHINDI wa mwisho wa MSIMU atashinda endapo tu atakusanya point nyingi Zaidi ya wengine kwa kujibu maswali ya mpira. Kila swali mteja atakalopokea atatozwa Tsh 99.
v)    Washiriki wote wa kampeni hii ni lazima wawe kuanzia miaka 18 na Zaidi.
vi)    Mteja anaweza kujiunga kwenye huduma kwa kutuma neno SOKA kwenda 15670. Kujiunga ni bure na baada ya hapo mteja atapokea maswali yanayohusu mpira. Kila swali atakalojibu litamgharimu TSH 99.
vii)    Neno lolote (isipokuwa A au B) litakalotumwa kwenye namba 15670 litajumuishwa kama jibu lisilo sahihi kwa swali lililopita. Mfumo utatuma SMS ya swali linalofuata kama mteja ana salio la kutosha.
viii)    Kila jibu sahihi mteja atapokea point MIA MOJA (100) na lisilo sahihi mteja atapokea point Ishirini na tano (25)
ix)    Washiriki wote wanaweza kupokea swali la awali muda wowote wa siku pindi watakapokuwa na salio kwenye simu zao ili kuwahimiza kucheza na kupata nafasi ya kushinda zawadi.
x)    Ili kupata nafasi ya kushinda, mteja anapaswa kujibu maswali ya mpira kuongeza nafasi yake ya ushindi.
xi)    Mteja anapojibu maswali mengi zaidi ndio anajiongezea pointi na anapata nafasi ya kujiongezea USHINDI.
xii)    Washiriki wote wa kampeni wana nafasi sawa ya KUSHINDA, Ukijibu Zaidi ndio unajiongezea nafasi ya KUSHINDA kwenye kila droo.
xiii)    Auto-renewal inamaanisha kila siku mteja atatozwa kiasi flani bila kutaarifiwa kwajili ya kubakia kwenye huduma na atakuwa na nafasi ya kujibu swali 1 bure na asipotumia nafasi hii kwa siku usika hakuna pande yoyote ya kuilaumu!
xiv)    Kujitoa katika huduma mteja anatakiwa kutuma neno ONDOA SOKA kwenda 15670 bure.
xv)    Washindi wote watapigiwa simu kujulishwa kuhusu ushindi wao. Mshindi yeyote ambaye hatopokea simu/Simu yake Haitopatikana kipindi cha kujulishwa Mshindi mara 3 ama atapokea na kutoonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi zinazotakiwa basi nafasi hiyo ITAONDOLEWA kwake na droo nyingine kufanyika ili kumpata mshindi mwingine.
xvi)    Mshindi yeyote ambaye alipigiwa simu na hakupatikana/ hakupokea simumara 3 ama kutoa taarifa sahihi zinazotakiwa hatokuwa na ruhusa ya kudai Zawadi hiyo.
xvii)    Zawadi zote za kampeni ya “SOKA SMS TRIVIA PROMOTION” zitakabidhiwa katika office za Tigo. 
xviii)    Kila mteja ananafasi ya kushinda Zawadi ya KIPENGELE FULANI MARA MOJA (1) tu na hairuhusiwi kushinda kipengele hicho tena. Mfano. Mteja akishinda Zawadi ya WIKI ya kwanza, hafai kushinda Zawadi ya wiki kwa wiki zinazofata.
xix)    Tigo itabakia na Zawadi ya Mshindi kwa muda wa miezi mitatu (3) endapo Mshindi huyo hajajitokeza kuichukua Zawadi yako. Baada ya muda huo Mshindi hatokuwa na haki ya kuichukua Zawadi. 
xx)    Tigo inaweza kutumia baadhi ya taarifa kama picha, sauti au video za MSHINDI aliyeshinda zawadi ya kampeni hii kwa kipindi chote cha kampeni kwa ajili ya uhamasishaji wa kampeni.
xxi)    Jina la Mshindi linaweza kuchapishwa kwenye magazeti au vyombo vingine vya habari. 
xxii)    Waajiriwa wa Green Telecom na Tigo pamoja na familia zao hawaruhusiwi ya kushiriki kwenye kampeni hii.
xxiii)    Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wote wa Tigo ambao ni raia wa Tanzania.
xxiv)    Majina ya washindi yanaweza kutangazwa au kuchapishwa katika vyombo vya habari vilivyochaguliwa na waendesha kampeni.
xxv)    Zawadi katika kampeni hii hairuhusiwi kubadilishana, kubadilishwa kwa kupewa mtu mwingine.
xxvi)    Washindi wote wanapaswa kutoa vitambulisho halali. Vitambulisho vifuatavyo kujumuishwa ( Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha mpiga Kura au Leseni ya Udereva) 
xxvii)    Tigo inauwezo wa kubadilisha vigezo na masharti muda wowote kwa kupeleka mapendekezo yao katika Taasisi ya Kuratibu Mashindano ya Bahati Nasibu (Gaming Board of Tanzania)

2.    Jinsi ya kuchagua washindi:
(i)    Kila wiki zawadi zitatolewa kwa washindi baada ya kushiriki kwenye kampeni kwa kupitia namba husika ya SMS (15670) na kukusanya point Zaidi ili kuingia kwenye droo.
(ii)    Muwakilishi wa Idara ya Bahati Nasibu (Gaming Board) lazima awepo pindi Mshindi anapotafutwa/kutajwa au kupigiwa simu.
(iii)    Kila unavyozidi kujibu maswali ndio unayojiongezea point na nafasi ya kuingia kwenye DROO ya ushindi.
(iv)    Mshindi wa wiki atakuwa ni yule atakaobahatika kati ya namba 30 zilizokusanya alama nyingi kwa kipindi cha wiki husika (Siku 7) na kushinda baada ya kufanyiwa droo.
(v)    Mshindi wa Msimu ni yule atakaebahatika kati ya namba 20 zilizokusanya ALAMA nyingi Zaidi kwa kipindi cha Msimu Mzima (Siku 90) na kufanyiwa droo.
(vi)    Mshindi wa siku ni yule atakaye kusanya alama nyingi zaidi ndani ya siku husika.
(vii)    Mshindi wa Safari ya Kwenda Ivory Coast atapaswa kuwa na Pasi ya kusafiria (Passport). Kukosa Pasi ya kusafiria kutafanya mteja kupoteza nafasi yake ya ushindi.


3.    ZAWADI;

i)    ZAWADI YA MWISHO WA MSIMU:                                                                                                   
Kutakuwa na Mshindi mmoja (1) wa zawadi ya mwisho wa msimu atakae zawadiwa Tsh 10,000,000 (Milioni Kumi tu).

ii)    ZAWADI ZA WIKI;
Kutakuwa na mshindi mmoja tu wa wiki (1) ambaye atashinda Tsh 200,000 (Laki mbili tu) Jumla ya washindi wa Wiki watakuwa 12 ndani ya msimu mzima.

iii)    ZAWADI ZA SIKU:
Kila siku kutakuwa na washindi 1 wa Tsh 50,000 (Elfu kumi) kila siku  kwa muda wa siku 90 za Msimu. 

iv)    Jezi: Jezi 45 zitatolewa kama Zawadi kwa washindi tofauti tofauti.

4.    UPATIKANAJI WA TAARIFA MUHIMU WA KAMPENI
A.    Taarifa zote muhimu kuhusu kampeni zinaweza kupatikana katika tovuti rasmi ya mtandao wa Tigo na kurasa zake za kijamii Pamoja na kurasa maalum ya Soka.
•    Instagram: sokaupdate
•    Facebook: sokaupdate
•    Website: tigo.co.tz
B.    Endapo kampeni itafika mwisho, wahusika wa kampeni watatoa taarifa rasmi kwa wateja kupitia vyanzo rasmi vya taarifa na wateja watapokea ujumbe mfupi.
C.    Usitishwaji au ukatizwaji wa kampeni hakumpi nafasi mtoa huduma ya kuyaacha majukumu yake ya kutoa zawadi zilizokwisha tangazwa isipokuwa pindi tu Usitishwaji au ukatizwaji wa kampeni uko nje ya uwezo wa mtoa huduma.
D.    Mtoa huduma wa Kampeni hana ruhusa ya kutoa taarifa yoyote ya washiriki wa mchezo ISIPOKUWA ikihitajika kufanywa hivyo kisheria.
E.    Mtoa huduma ana haki ya kutoingia kwenye mazungumzo ya maandishi au kuwasiliana na washiriki isipokuwa kwa mujibu wa Kanuni na Masharti au kwa mujibu wa mahitaji ya sheria Tanzania ya sasa.
F.    Ni wajibu kwa mtoa huduma kuhakikisha namba ya huduma “short code” inapatikana/inafanya kazi kwa akipindi chote cha kampeni.


5. UKOMO WA KUPOKEA TAARIFA ZA MCHEZO/KAMPENI 
Uhesabuji wa taarifa zote za siku za mchezo utafanyika mwisho wa siku (SAA 5:59:59).

6. KUSITISHWA KWA HUDUMA AU MASHARTI YA MATUMIZI.
Endapo kutakuwa na usitishwaji wa huduma au moja ya matumizi ya masharti kwa hiyari yetu, taarifa inaweza kutolewa kwenu kwa kupitia barua, barua pepe, kupigiwa simu (Kwa ujumbe uliorikodiwa au ujumbe mfupi sms) kupitia machapisho ya kila siku au ya kila wiki au kuchapishwa kupitia tovuti yetu rasmi. Unashauriwa kutembelea tovuti yetu mara kwa mara iili kuengalia kama kuna machapisho ya mabadiliko yeyote ambayo yanaweza kutowafikia kwa matatizo ambayo yapo nje ya uwezo.