10 Mar 2025 / 68 views
Amorim amwagia sifa Fernandez

Kocha mkuu wa Manchester United Ruben Amorim anahisi klabu hiyo isingekuwa katika hali mbaya kama ingekuwa na wachezaji wengi kama Bruno Fernandes.

Nahodha huyo wa United aliongoza kutoka mbele katika sare ya 1-1 na Arsenal Uwanja wa Old Trafford.

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta alikiri Mreno huyo "alikuwa mwerevu sana kwetu na kwa mwamuzi" kwa jinsi alivyobadilisha nafasi ya mpira wake wa adhabu katika kipindi cha kwanza ili kumpa nafasi nzuri ya kuiweka United mbele.

Mpira ulipimwa kuwa umbali wa yadi 11.2 kutoka kwa ukuta baada ya mechi, badala ya yadi 10 ambazo sheria zinasema unapaswa kuwa.

Kipa wa zamani wa Newcastle Shay Given aliiambia BBC Mechi Bora ya Siku: "Ulikuwa ni mchezo mzuri sana, lakini ndio ukuta ulikuwa nyuma sana.

"Labda mwamuzi aliihesabu vibaya, lakini inampa Bruno faida hiyo. Mpira ukiwa umbali wa yadi 11, Bruno anaweza kuupiga kwa kasi zaidi."

Nahodha wa zamani wa United Roy Keane anaweza kuwa asiwe shabiki wa Fernandes kutokana na jinsi raia huyo wa Ireland alivyozungumza kuhusu Fernandes.