
Tetesi za usajili
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wa Uingereza Jack Grealish, 29, huku kukiwa na mipango ya kukimarisha kikosi cha City.
Inter Milan wanaibuka wapinzani wakuu wa klabu ya Liverpool katika mbio za kumsajili kiungo wa Ujerumani Joshua Kimmich huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akiingia akisalia na miezi michache katika mkataba wake na Bayern Munich.
Chelsea inamfuatilia kwa karibu kipa wa Uholanzi na klabu ya Brighton Bart Verbruggen, 22, kwa ajili ya uhamisho wa majira ya joto.
Manchester United, Tottenham na Arsenal zimeonyesha nia ya kumsajili Benjamin Sesko kutoka RB Leipzig, na mshambuliaji huyo wa Slovenia mwenye umri wa miaka 21 ana kipengele cha kutolewa ambacho kinaweza kutumika msimu huu wa joto.
Mshambuliaji wa Canada Jonathan Davidyuko tayari kuondoka katika klabu hiyo kama mchezaji huru msimu huu wa joto.
Wasaka vipaji wa Real Madrid wamekuwa wakimfuatilia kiungo wa England Adam Wharton tangu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 arejee kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Crystal Palace.
Liverpool wameanza mazungumzo na Conor Bradley kuhusu kandarasi mpya ya miaka mitano ambayo itamuwezesha beki huyo wa Ireland Kaskazini, 21, kupata nyongeza ya 650%.
Brentford na Fulham zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Mexico Johan Vasquez, 26, kutoka Genoa.
Fulham na Sporting wanamuwinda beki wa Ugiriki, Georgios Vagiannidis, huku Sporting wakiwasilisha dau la euro 10m (£8.3m) kwa Panathinaikos.
Beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 29, ataondoka Bayer Leverkusen kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.
Gwiji wa zamani wa a Atletico Madrid Andrea Berta anaaminika kuwa miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya Edu kama mkurugenzi wa michezo wa Arsenal.