12 Mar 2025 / 63 views
Tetesi za usajili

Mshambuliaji wa Brazil, Vinicius Jr, atakuwa na fursa ya kuhamia ligi kuu ya Saudi Arabia kwa pauni milioni 200 msimu wa joto, wakati atakapokuwa imesalia miaka miwili kwenye mkataba wake na Real Madrid.

Atletico Madrid wanasaka mshambuliaji mpya msimu huu wa joto, na miongoni mwa majina waliyonayo yumo mshambuliaji wa Liverpool, Darwin Nunez, mwenye umri wa miaka 25.

Liverpool watamuuza Nunez ikiwa tuwatapata mbadala wake, huku mshambuliaji wa Brighton, Joao Pedro, mwenye umri wa miaka 23, akiwa miongoni mwa majina yaliyo kwenye orodha ya inayowafukuzia.

Tottenham huenda wakafanya harakati za kumsajili mchezaji wa Crystal Palace, Eberechi Eze, msimu huu wa joto, baada ya kuwa "chaguo halisi" kwa winga huyo wa England, mwenye umri wa miaka 26.

Manchester City wanafikiria kumsajili beki wa kushoto wa Ufaransa, Theo Hernandez, msimu huu wa joto, huku mazungumzo yake ya mkataba mpya na AC Milan yakiwa yamesimama. Hernandez ana umri wa miaka 27.

AC Milan wamemtaja beki wa kushoto wa Wolves, Rayan Ait-Nouri, mwenye umri wa miaka 23, kama mbadala anayetarajiwa wa Hernandez.

Samu Aghehowa wa Porto ameibuka kuwa chaguo mahususi la usajili kwa Aston Villa, huku mshambuliaji huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 20 akiendelea kuwavutia pia Chelsea, Arsenal na West Ham.

Kocha mpya wa West Ham, Graham Potter, ameelekeza macho yake kwa mshambuliaji wa Canada, Jonathan David, mwenye umri wa miaka 25, kutoka Lille, huku akipambana na klabu kama Barcelona kupata saini yake.

Manchester United watalazimika kulipa jumla ya pauni milioni 20 kwa kocha Ruben Amorim na benchi lake la ufundi iwapo klabu itaamua kumfuta kazi.