03 Mar 2025 / 87 views
Tetesi za soka Ulaya

Jamie Gittens atazigharimu klabu za ligi kuu England karibu £85m, wakati huu Manchester United ikikutana na kikwazo katika mbio zao za kumnasa Victor Osimhen huku wenzao Manchester City wakiingia katika mbio za kumnasa kiungo huyu kinda mwenye kipaji.

Manchester United wanamtaka Victor Osimhen, ambaye yuko kwa mkopo Galatasaray kutoka Napoli, lakini matamanio ya mnigeria huyo mwenye miaka 26 kucheza klabu bingwa Ulaya na mshahara mkubwa inaweza kukwamisha mpango huo.

Kiungo wa Manchester United, Mbrazili Casemiro, 32, anataka kumalizia mkataba wake wa miezi 16 uliosalia anaolipwa £300,000 kwa wiki, ambapo unavuruga mpango wa klabu yake kumpiga bei ili kutunisha mfuko wake wa usajili.

Nia ya Manchester City kumnasa nyota wa Bayer Leverkusen na kiungo wa Ujerumani Florian Wirtz, 21, inayoweza kuwagharimu zaidi ya £85m, inaongezeka makati huu klabu hiyo inajiandaa na kuondoka kwa mbelgiji Kevin de Bruyne.

Borussia Dortmund inataka £85m (102m euros) kuumuza Jamie Gittens, huku vilabu vya Arsenal, Tottenham na Chelsea ni miongoni vilabu vinamyomtakka winga huyo wa kimataifa wa Engand U21.

Katika dirisha lijalo la majira ya joto, Manchester City itapokea ofa kwa ajili ya kiungo wake mreno Bernardo Silva, huku klabu za Hispania, Ureno, na Saudi Arabia zikionyesha nia ya kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 30.

Mshambuliaji kinda wa Argentinia, Claudio Echeverri, 19, atajiunga na kikosi cha Manchester City wiki hii, baada ya kutumia mwaka uliopita kukipiga kwa mkopo kwenye klabu ya River Plate.

Manchester City itakutana na upinzani kutoka kwa mahasimu wao Manchester United katika hekaheka za kumnasa kiungo mbelgiji wa Atalanta Charles de Ketelaere.