11 Feb 2025 / 104 views
Tetesi za soka Ulaya

Mpango wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Mathys Tel watibuka huku Arsenal wakisubiri pembeni, beki wa Chelsea Axel Disasi anawindwa naye Joao Felix anasakwa na AC Milan na Aston Villa.

Mshambuliaji wa Ufaransa Mathys Tel, 19, anataka kujiunga na Manchester United lakini mazungumzo ya kufanikisha azama hiyo na Bayern Munich yametibuka kwa sasa, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka aondoke uhamisho wa kudumu.

Manchester United wanamtaka Tel, lakini mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, ni chaguo jingine katika siku ya mwisho. (ESPN)

Arsenal wanasubiri kwa hamu baada ya ofa mbili zilizowasilishwa na United kumsajili Tel kukataliwa siku ya Jumapili.

Tottenham wamekubali Chelsea kumsajili mkataba wa mkopo na mlinzi Axel Disasi, 26, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anataka kuhamia Aston Villa.

Beki wa kushoto wa Chelsea na England Ben Chilwell, 28, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Crystal Palace, kabla ya kuhamia klabu hiyo kwa mkopo siku ya mwisho wa uhamisho wa wachezaji.

Newcastle itamruhusu mlinzi wa Uingereza Lloyd Kelly, 26, kuelekea Juventus katika mkataba ambao utafanywa wa kudumu msimu wa joto.

Joao Felix anatarajia kuondoka Chelsea siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji huku klabu za AC Milan na Aston Villa zikiwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 25.