19 Sep 2024 / 84 views
Palmer na Chilwell waacha Conference

Cole Palmer na Ben Chilwell ni miongoni mwa wachezaji wanne waandamizi walioachwa kwenye kikosi cha Chelsea cha Ligi ya Conference.

Mshambuliaji wa England Palmer, kiungo Romeo Lavia na mlinzi Wesley Fofana wameachwa kwa makusudi ili kudhibiti mzigo wao wa kazi.

Chelsea inaweza kucheza takriban mechi 80 msimu huu katika mashindano matano.

Uamuzi huo ulifanywa kumpumzisha nyota wake Palmer katika awamu ya ligi ya daraja la tatu barani Ulaya, huku Lavia na Fofana wakijaribu kurejea kutokana na majeraha ya muda mrefu.

Chelsea inaweza kusajili tena wachezaji watatu kwa raundi ya muondoano mnamo 6 Februari wakati vikosi vinaweza kuwasilishwa tena.