02 Sep 2024 / 11 views
Tetesi za soka Ulaya

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28. The Blues hata hivyo hawataweza kufikia mshahara unaopendekezwa na klabu ya Al-Ahli ya Saudi Arabia.

Toney anaweza kulipwa hadi £400,000 kwa wiki akiamua kujiunga na klabu hiyo ya Saudi Pro League.

Newcastle na Manchester United wanatazamia kumnunua mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 27, ambaye mkataba wake unamalizika Everton msimu ujao.

Liverpool wanawania kukamilisha usajili wa mshambulizi wa Juventus na Italia Federico Chiesa, 26, kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa Ijumaa.

Kiungo wa kati wa Lyon na Ubelgiji Orel Mangala, 26, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na Everton kwa nia ya kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji.

Leicester wanakaribia kufikia mafanikio katika ombi lao la pauni milioni 19.5 kumnunua kiungo wa kati wa Genk na Morocco Bilal El Khannouss, 20.

Nottingham Forest inamnyatia mshambuliaji wa Ajax na Uholanzi Brian Brobbey, 22, na huenda wakamsajiliwa kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa.

Chelsea watamsajili mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 20, endapo watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Napoli na timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen,25.

Roma wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 26, huku West Ham wakimtaka.

Bayern Munich na Borussia Dortmund wanafuatilia hali ya winga wa Uingereza Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 24 katika klabu ya Manchester United.

Manchester City bado hawajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wa kiungo wa kati wa Ureno Matheus Nunes, 25, lakini wanajua kuwa Atletico Madrid wana nia ya kumnunua.

Ipswich Town wamepiga hatua katika mpango wa kumsajili winga wa Jamhuri ya Ireland Chiedozie Ogbene, 27, kutoka Luton Town.

Leeds wameanza kujadiliana na Fortuna Düsseldorf kwa nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Japan Ao Tanaka, 25.

Bayern Munich wamefikia mkataba na Al-Hilal ya Saudi Arabia kwa ajili ya Kingsley Coman, hata hivyo winga huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 bado hajajitolea kuhama.