Tetesi za soka Ulaya
Chelsea wanamchukulia mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 27, kama chaguo la gharama nafuu zaidi kuliko Victor Osimhen, 25, wa Napoli kutokana na matakwa ya mshahara ya mshambuliaji huyo wa Nigeria.
Juventus wameomba Manchester United kulipa sehemu ya mshahara wa Jadon Sancho ili kusaidia kuwezesha uhamisho wa winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24.
Arsenal watamlenga mshambuliaji mwingine watakapokamilisha dili la kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Merino, 28, kutoka Real Sociedad.
Uhamisho wa mkopo wa Armando Broja kutoka Chelsea kwenda Ipswich unakaribia kusambaratika baada ya uchunguzi wa kimatibabu wa mshambuliaji huyo wa Albania mwenye umri wa miaka 22 kufichua dalili za jeraha.
Mshambulizi wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, ataondoka Chelsea ili kujiunga na Napoli kwa mkataba wa miaka mitatu.
Porto wamekamilisha usajili wa pauni milioni 12.7 wa mshambuliaji wa Uhispania Samu Omorodion, 20, kutoka Atletico Madrid - wiki chache tu baada ya pendekezo la uhamisho wa pauni milioni 33.9 kwenda Chelsea kusambaratika.
Nottingham Forest wana nia ya kumsajili Arnaut Danjuma kutoka Villarreal, huku mshambuliaji huyo wa Uholanzi, 27, akipendelea uhamisho wa kudumu badala ya uhamisho wa mkopo.