01 Aug 2024 / 84 views
Tetesi za soka Ulaya

Chelsea wanajadili mpango wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, kujiunga na Napoli, huku mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, akitarajiwa kuhamia klabu hiyo kwa mkopo.

Lukaku tayari amekubali kukatwa mshahara na kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Serie A.

Brighton wamekubali mkataba wa pauni milioni 5.9 kumruhusu kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross, 33, kujiunga na Borussia Dortmund. 

Chelsea na Aston Villa wamewasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Maximilian Beier, 21.

Uhamisho wa Monza kwa mlinda lango wa Nottingham Forest na Costa Rica Keylor Navas, 37, unaweza kutibuka kutokana na tofauti kati ya pande hizo mbili wakati wa mazungumzo.

Chelsea pia wamefikia mkataba wa pauni milioni 16.7 na Genk kwa ajili ya mlinda lango wa Ubelgiji Mike Penders, 18.

West Ham wanataka kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kumnunua winga wa Leeds ya Uholanzi Crysencio Summerville

Aston Villa wanavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 27.

Everton wanafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Roma Muingereza Tammy Abraham, 26.

Manchester United wanajitahidi kufikia makubaliano na kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye aliondoka Juventus msimu huu wa joto.

Beki wa England chini ya miaka 21 Rhys Williams, 23, na mlinzi wa Ufaransa Billy Koumetio, 21, wanatarajiwa kuondoka Liverpool.