
Fullkrug kutua West Ham
West Ham wamefanya mazungumzo na Borussia Dortmund kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Niclas Fullkrug.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alifunga mara mbili kwenye michuano ya Euro 2024 wakati wenyeji walipotinga robo fainali na ni miongoni mwa chaguzi zinazolengwa na mkufunzi wa Wagonga nyundo Julen Lopetegui.
West Ham wana nia ya kuongeza nguvu zaidi kwenye safu yao ya ushambuliaji na wako kwenye mazungumzo ya wachezaji wengi, akiwemo fowadi wa Aston Villa wa Colombia Jhon Duran.
Fullkrug alifunga mabao 16 katika mechi 46 alizoichezea Dortmund msimu uliopita baada ya kuhama kutoka Werder Bremen kwa mkataba wa £12.6m na kuisaidia klabu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa ambapo walishindwa na Real Madrid.
The Hammers pia wanataka kumsajili beki wa pembeni Aaron Wan-Bissaka kutoka Manchester United.
Walimsajili nahodha wa Wolves Max Kilman kwa £40m mwezi uliopita, na kipa Wes Foderingham na winga wa Brazil Luis Guilherme pia wamejiunga na klabu msimu huu wa joto.