Tetesi za soka Ulaya
Arsenal bado wanamtaka mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen.
Napoli pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, na huenda wakamjumuisha katika mkataba wa kubadilishana na Osimhen.
Mlinzi wa Jamhuri ya Ireland Jake O'Brien, 23, amewasili Merseyside kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya uhamisho wake wa pauni milioni 17 kutoka Lyon kwenda Everton.
Everton huenda wakawasilisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Strasbourg na Senegal Habib Diarra, 20.
Vilabu kadhaa kutoka Ligi ya England na nje ya nchi vinawania kumsajili winga wa Luton Mholanzi Tahith Chong, 24, kwa takriban £10m.
West Ham wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa na Monaco Youssouf Fofana, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anavutiwa na klabu ya AC Milan.
Kipa wa zamani wa Manchester United David de Gea, 33, hatajiunga na Genoa, na Mhispania huyo hakuwahi kukaribia kujiunga na klabu hiyo ya Italia.
West Ham wameelekeza darubini yao kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Niclas Fullkrug, 31, wanapomtafuta mshambuliaji mpya.
Arsenal wanavutiwa na winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 hana nafasi ya kuhama msimu huu wa joto.