30 Jul 2024 / 112 views
Alvarez kuhamua hatma yake

Mshambuliaji wa Manchester City, Julian Alvarez anasema atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo baada ya Michezo ya Paris 2024.

Alvarez, 24, anatarajiwa kuanza kwa mara ya tatu kwa Argentina kwenye Michezo ya Olimpiki watakapomenyana na Ukraine Jumanne mjini Lyon.

Mnamo Machi 2023, Alvarez alisaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja ili kumbakisha City hadi 2028.

"Kuna mazungumzo mengi," alisema Alvarez kabla ya mechi ya Ukraine alipoulizwa kuhusu mustakabali wake wa City.

"Ninalenga hapa [kwenye Olimpiki] kwa sababu ni mashindano mafupi. Nikiwa Manchester City najisikia vizuri sana, nilicheza kwa dakika nyingi.

"Lakini tutaona baada ya Michezo. Kwanza, nikiweza, nitachukua siku chache za mapumziko. Kisha tutaamua."