
Tetesi za soka Ulaya
Juventus wanataka kumuuza fowadi wa Italia Federico Chiesa, 26, ili kupata fedha za kumnunua winga wa Manchester United Jadon Sancho, huku klabu hiyo ya Italia ikifanya mazungumzo kuhusu aina ya ofa ya kumpa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 24.
Kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, amekamilisha matibabu yake na Bayern Munich lakini anahitaji kufafanua baadhi ya maelezo na Fulham kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa euro 46m.
Kiungo wa kati wa Uhispania Aleix Garcia, 27, anasema West Ham ilijaribu kumsajili kutoka Girona lakini alichagua kujiunga na Bayer Leverkusen badala yake.
Real Betis wamefikia makubaliano na Leeds United kumsajili beki wa Uhispania Diego llorente, 30, kutoka klabu ya Elland Road.
Manchester United watafanya mkutano kuhusu uhamisho wa wachezaji siku ya Jumatatu ambao utajumuisha uamuzi kuhusu iwapo watatoa ofa nyingine kwa Everton kumsajili mchezaji mwenye umri wa miaka 22 na beki wa kati wa England Jarrad Branthwaite.
Mshambulizi wa Manchester United Mason Greenwood anataka mustakabali wake utatuliwe wiki ijayo, huku Atletico Madrid, Barcelona, Juventus, Lazio, Marseille na Valencia - ambao wamewasilisha ombi la pauni milioni 25 - wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 22.
Manchester City wamesajili nia ya kutaka kumnunua winga wa Newcastle United na Uingereza Anthony Gordon, 23, ambaye mkataba wake unamalizika Juni 2026.
Beki wa Ureno Joao Cancelo, 30, amepewa ofa kwa Inter Milan na Juventus baada ya kurejea Manchester City kufuatia kukamilika kwa muda wake wa mkopo Barcelona.
Real Madrid itasubiri hadi beki wa kushoto wa Bayern Munich Alphonso Davies amalize kucheza Copa America na Canada kabla ya kujaribu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 katika dirisha hili la usajili au kuamua kama asubiri hadi msimu ujao wakati atakuwa mchezaji huru.
Bayern Munich itapata euro 20m ikiwa Manchester United itaanzisha kifungu cha kutolewa cha euro 40m cha mshambuliaji wa Bologna Joshua Zirkzee baada ya kuingiza kifungu cha 50% cha mauzo walipomuuza Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa klabu hiyo ya Italia.