10 May 2024 / 102 views
Ferguson kiungo bora Seria A

Mchezaji wa kimataifa wa Scotland, Lewis Ferguson ametunukiwa Tuzo ya Nambari 8 ya Bulgarelli, iliyotolewa kwa kiungo bora wa Serie A kwa msimu huu.

Nahodha huyo wa Bologna alikuwa na msimu mzuri sana huku timu yake ikiwinda kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, kabla ya kupata jeraha la goti lililomaliza kampeni mwezi Aprili.

Kabla ya kipigo hicho, Ferguson alikuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri kwenye ligi kuu ya Italia, akifunga mara sita na kusajili pasi nne za mabao katika mechi 31 za ligi.

Washindi wa awali wa tuzo hiyo ni pamoja na Daniele De Rossi, Nicolo Barella na Sandro Tonali.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atakosa michuano ya Euro mwaka huu nchini Ujerumani baada ya kufanyiwa upasuaji.