
Messi afunguka kucheza ligi ya Marekani
Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi amesema kuwa nia yake ilikuwa ni Kwenda ligi kuu ya Marekani katika timu ya Inter Miami baada ya kuachana na Paris St Germain.
Messi amecheza mechi yake ya mwisho kwa PSG wiki iliyopita alihusishwa na kujiunga na Barcelona Pamoja na ligi ya Saudi Arabia.
"Nimefanya maamuzi naenda Miami’ Messi amesema kwenye mahujiano wakati wa kuwaaga mashabiki wake wa PSG.
Hii ni mara ya kwanza kwa Lionel Messi kucheza ligi nje ya Ulaya toka alipojiunga na Barcelona ya vijana akiwa na umri wa miaka 13 na kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi katika La Liga akifunga magoli 672.
Messi ameiongoza Argentina kushinda kombe la Dunia mwezi Desemba 2022 nchini Qatar ameshinda Ballon d’Or sab ana ameshinda kombe la Ligi akiwa na PSG katika misimu yake miwili Pamoja kombe Ufaransa 2022.
"Baada ya kushinda Kombe la Dunia na kutoweza kwenda Barca, ulikuwa wakati wa kwenda kwenye ligi ya Amerika ili kupata uzoefu wa kandanda kwa njia tofauti na kufurahiya kila siku," Messi alisema.
"Ni wazi kwa jukumu sawa na hamu ya kutaka kushinda na kufanya mambo vizuri kila wakati. Lakini kwa amani zaidi ya akili."