
Inter Miami wamtaka Messi
Inter Miami wamempa Lionel Messi ofa ya euro 50m kwa mwaka (£42.9m) ili kuitumikia klabu hiyo ya MLS kwa miaka minne baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 35, kuondoka Paris St-Germain msimu huu.
Mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 35, atajiunga na klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad mara mkataba wake wa Real Madrid utakapokamilika mwezi huu.
Kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 37, pia ameiambia Real Madrid kuwa anatarajia kuikubali ofa ya euro 120m (£103m) ili kucheza Saudi Arabia kwa misimu mitatu ijayo.
Newcastle wanajiandaa kupambana na Manchester United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, kutoka Napoli.
Kiungo wa kati wa West Ham ya England Declan Rice angependelea kusalia kwenye Ligi kuu ya England msimu huu wa joto anapojiandaa kukataa kuhamia Bayern Munich, huku Arsenal na Manchester United zikimtaka zaidi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.
Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, 29, kutoka Chelsea.
Bosi wa Celtic raia wa Australia Ange Postecoglou anaweza kuthibitishwa kuwa meneja mpya wa Tottenham mapema wiki ijayo.
Kocha Muingereza Sam Allardyce, 68, hatapewa mkataba mpya wa kusalia Leeds baada ya kushindwa kufanya vyema katika mechi zake nne alizopewa za mwisho mwa ligi ili kuinusuru timu hiyo isishuke daraja.
Joao Cancelo wa Manchester City kuna uwezekano mkubwa wa kufanya uhamisho wake wa mkopo kwenda Bayern Munich kuwa wa kudumu msimu huu wa joto.
Beki huyo wa pembeni wa Ureno, 29, hataki kurejea England - kuichezea Arsenal wanaomtaka na ambao wamemaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi.
Bayern wanatazamiwa kutoa ofa kwa mawinga wa Ujerumani Serge Gnabry na Leroy Sane, wote wana miaka 27, msimu huu wa joto, pamoja na mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane - mwaka mmoja tu baada ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 31 kutoka Liverpool.
Chelsea wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka kwa Brighton kwa ajili ya kumnunua beki Mwingereza Levi Colwill, 20, ambaye ametumia msimu huu kucheza kwa mkopo akiwa na Seagulls.
Wolves wameungana na West Ham, Newcastle na Aston Villa kutaka saini ya kiungo wa kati wa Southampton Muingereza James Ward-Prowse.