03 Jun 2023 / 88 views
Haaland aapa kuwapa Man City treble

Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland amesema kuwa atafanya kila kitu kuisadia timu yake hiyo kushinda makombe matatu msimu huu.

City imeshinda ubingwa wa ligi kuu soka nchini England EPL na wanaweza kuongeza makombe mengine mawili kama wataifunga Manchester United kwenye fainali ya kombe la FA Pamoja na Inter kwenye fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

United walishinda mataji yote matatu mwaka 1999 na kuwa timu pekee kutoka England kushinda mataji matatu msimu mmoja.

Licha ya utawala wa ndani wa City, bado hawajashinda Ligi ya Mabingwa na Haaland anatumai kuwa anaweza kukosa kupata mafanikio katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka barani Ulaya.

"Inamaanisha kila kitu. Nitafanya kila niwezalo kujaribu kuifanya itimie. Ni ndoto yangu kubwa na natumai ndoto zitatimia."

Aliongeza: "Lakini vile vile sio rahisi - ni fainali mbili dhidi ya timu mbili nzuri ambazo zitafanya kila wawezalo kujaribu kuharibu hilo.

"Watakuwa na motisha, watakuwa tayari na lazima tucheze kwa ubora wetu, kwa sababu tukicheza kwa ubora wetu tuna nafasi kubwa ya kufikia hilo."

City iliipiku Arsenal msimu huu na kushinda taji la tatu la Premier League mfululizo chini ya meneja Pep Guardiola.