
Tetesi za soka Ulaya
Newcastle wamempa Bruno Guimaraes mkataba mpya wenye mshahara pauni 200,000 kwa wiki ili asiende Liverpool, Real Madrid au Barcelona zinazomtaka na kumfanya kiungo huyo wa kati wa Brazil, 25, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Liverpool wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 24, kuhusu maslahi binafsi na wanatarajia kukamilisha usajili wake kutoka Brighton wiki ijayo.
Joao Felix atapelekwa Newcastle kwa mkopo na klabu mama Atletico Madrid siku chache tu baada ya Chelsea kutangaza kutomsajili mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 kwa uhamisho wa kudumu.
Ruben Loftus-Cheek, 27, amekubali kuondoka Chelsea na kwenda AC Milan huku klabu hiyo ya Serie A ikitayarisha ofa ya £13m kwa kiungo huyo wa kati wa England.
Nahodha wa England Harry Kane, 29, anataka kuhamia Manchester United msimu huu wa joto, badala ya kuhamia nje ya nchi, lakini yuko tayari kumaliza mkataba wake na kuondoka Tottenham kama mchezaji huru mwaka ujao.
Real Madrid wanaweza kumnunua Kane iwapo mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 35, atakubali ofa nono aliyotangaziwa huko Saudi Arabia.
Tottenham itaongeza harakati za kumnunua Ange Postecoglou baada ya timu yake ya Celtic kucheza fainali ya Kombe la Scotland Jumamosi.
Chelsea wanataka kumuuza beki wa kati wa Senegal Kalidou Koulibaly, 31, ambaye alisajiliwa kwa pauni milioni 33 kutoka Napoli msimu uliopita wa joto.
Chelsea pia imetoa ruhusa kwa Manchester City kuanza mazungumzo na kiungo wao wa kati wa Croatia Mateo Kovacic.
Manchester United, Barcelona na Inter Milan wana nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Ufaransa Benjamin Pavard, 27, ambaye hataki kuongeza mkataba mpya pale Bayern Munich, wa sasa unakakamilika 2024.
Yasser Al-Misehal, rais wa Shirikisho la Soka la Saudi Arabia, anasema "binafsi" angependa kumuona Muargentina anayehusishwa na Al-Hilal Lionel Messi, 35, akicheza katika Ligi ya Pro ya nchi hiyo na kama alivyofanya Cristiano Ronaldo, 38 aliyehamia Al Nassr mwezi Januari.
Muda wa Sam Allardyce kama meneja wa Leeds unatarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi, wakati bosi huyo wa zamani wa Bolton na West Ham anatarajiwa kukutana na uongozi wa klabu hiyo.
Arsenal wametoa ofa ya kuongeza mshahara wa William Saliba mara tatu zaidi katika mkataba mpya wenye thamani ya £120,000 kwa wiki, lakini wanahofia kumpoteza beki huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 kwenda Paris St-Germain.