26 May 2023 / 88 views
Dortmund wakaribia ubingwa

Klabu ya Borussia Dortmund watashinda ubingwa wa Bundesliga baada ya miaka 11 kama waifunga Mainz kwenye mechi ya mwisho ya ligi hiyo.

Dortmund wapo mbele kwa alama mbili dhidi ya Bayern Munich kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini Ujerumani.

Bayern watacheza dhidi ya FC Koln kwenye mechi ya mwisho ya ligi ambao nao wanahitaji kushinda mechi hiyo huku wakiwaombea Dortmund kufungwa au kudroo kwenye mechi yao dhidi ya Mainz.

"Hatuwezi kuruhusu hili litokee kwetu, Alisema mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund, Sebastian Kehl.

Kehl ambaye aliiongoza Dortmund kushinda taji la Ujerumani msimu wa 2011-12 chini ya kocha wa sasa wa Liverpool, Jurgen Klopp.

"Kimsingi nina hisia nzuri, lakini najua kwamba tunapaswa kufanya vizuri mara moja zaidi na ndipo tutastahili.

"Wachezaji wanapopanda basi kwenda uwanjani watashangiliwa na umati wa watu. Hiyo itawasukuma."

Ingawa imekuwa mbio za ubingwa hadi sasa, huku Dortmund na Bayern zikishiriki katika kilele mara kadhaa, ikiwa timu ya Edin Terzic inaweza kumaliza kazi itashinda ushindi wa ajabu.