26 May 2023 / 92 views
Manchester United yafuzu UEFA

Manchester United imefuzu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya UEFA baada ya kuwafunga Chelsea 4-1 kwenye mechi iliyofanyika uwanja wa Old Trafford.

Casemiro alianza kuwaweka wenyeji mbele huku goli la pili likifungwa na Anthony Martial akipokea pasi kutoka kwa Jadon Sancho na kufanya matokeo kuwa 2-0 kipindi cha kwanza.

Bruno Fernandes aliiandikia Manchester United goli la tatu kwa penati baada ya kuwafanyiwa faulo na na beki wa Chelsea, Wesley Fofana.

Kosa lingine kutoka kwa Fofana likaigharimu timu yake baada ya kufanya makosa eneo la hatari na Manchester United kuandika goli la nne kupitia mshambuliaji wake, Marcus Rashford.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Manchester United imefuzu kucheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao na kuwapiku Liverpool.

Ilikuwa sio Habari nzuri kwa mchezaji wa Brazil, Anthony ambaye alibebwa kwa machela kutokana na kuumizwa na beki wa Chelsea, Trevor Chalobah.

Meneja Erik ten Hag alisema: “Ninaweza kukuambia kuwa ni mbaya lakini tunapaswa kusubiri angalau saa 24 na kisha tujue zaidi kuhusu hali ya jeraha lake."

Kwa Chelsea, msimu wao wa masikitiko - mbaya zaidi katika takriban miongo miwili - hauwezi kumalizika haraka vya kutosha, ingawa mashabiki wao angalau wamehifadhi hisia zao za ucheshi walipoimba "tumefunga bao" walipokuwa wakisherehekea juhudi za Felix.