26 May 2023 / 60 views
Mane kuondoka Bayern Munich

Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich, Lothar Matthäus amesema kuwa mahusiano ya Sadio Mane na Bayern Munich yamefikia mwisho.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal alijiunga na Bayern Munich kwa dau la paundi milioni 35 akitokea Liverpool msimu uliopita.

Mane amekuwa na misukosuko toka alivyojiunga na mabingwa hao wa Ujerumani kutokana na kusumbuliwa na majeruhi na kutokuwa na maelewano na wachezaji wenzake.

“Uhusiano kati ya Bayern Munich na Sadio Mane umekwisha. Labda uhusiano ulikuwa wa makosa, labda moja ya makosa mengi ambayo Bayern wamefanya katika miezi 12 iliyopita,” alisema kwenye mahojiano.

Sadio Mane ameichezea Bayern Munich mara 38 katika michuano yote tangu ajiunge nayo na kufunga mabao 12 na asisti 5.

Bayern kwa sasa wako nafasi ya pili kwenye jedwali la Bundesliga wakiwa na pointi 2 wakiwatenganisha na viongozi wa Borussia Dortmund.