25 May 2023 / 59 views
Ten Hag ataka Martial kubakia Man United

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amesema kuwa anahitaji Anthony Martial kubakia na kiwango chake na kufanya vizuri na klabu hiyo anapopatikana.

Martial amekosa mechi nyingi msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha lakini amecheza mechi 13 za Manchester United hivi karibuni kwenye michuano yote.

Ametengeneza jumla ya goli 16 katika mechi 74 alizocheza kwa Manchester United ambapo mchezaji huyo ana husishwa kujiunga na Aston Villa.

Man United wanatarajia kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji mpya kujiandaa na msimu ujao ambapo wanahusishwa na mshambuliaji wa Frankfurt Kolo Muani na Victor Osimhen wa Napoli.

Akizungumza kuelekea mechi ya ligi kuu dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Old Trafford, Ten Hag amesema kuwa anahisi timu yake inacheza vizuri kama Martial anapatikana kwenye mechi.

“Kama hautopatikana, huwezi kushinda, Amesema kocha huyo. Alipopatikana tumecheza vizuri timu inashinda’ Aliongeza kocha huyo

Man Utd inahitaji alama moja kwenye mechi zake mbili zilizobaki ili afanikiwe kumaliza nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini England.