25 May 2023 / 73 views
Tetesi za soka Ulaya

Manchester United hawana budi kulipa pauni milioni 140 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, msimu huu baada ya kuafikiana dili la mchezaji-mwenza na mlinzi wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26.

Napoli wanajaribu sana kumshawishi Kim kusaini mkataba mpya kabla ya kifungu cha kuachiliwa kuanza kutumika msimu huu wa joto.

Mikel Arteta yuko tayari kumruhusu kiungo wa kati wa Uingereza Emile Smith Rowe, 22, kuondoka Emirates ili kutoa nafasi kwa kiungo wa Leicester na England James Maddison,

The Gunners pia wana nia ya kumuongeza mshambuliaji wa Torino na Paraguay Antonio Sanabria, 26, kwa mkataba wa thamani ya £21.6m.

Mshambulzi wa Tottenham na England Harry Kane, 29, bado anasalia kuwa chaguo la kwanza la Manchester United na klabu hiyo inapania kuanza mapema kufanya mazungumzo na Spurs.

Real Betis huenda ikafufua nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Leeds United Mhispania Marc Roca, 26, ikiwa klabu hiyo ya Yorkshire itashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia.

Arsenal wamempa kiungo wa Uingereza Reiss Nelson mkataba mpya hadi 2027, inayojumuisha chaguo la nyongeza ya mwaka, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 pia amepokea ofa kutoka kwa timu zingine za Ligi ya Premia, Italia na Uhispania.

Martin, 37, amekubali mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja mpya wa Southampton, huku klabu hiyo iliyoshuka daraja ya Premier League ikitarajiwa kutangaza kuteuliwa kwake siku zijazo.