24 May 2023 / 69 views
Nistelrooy ajiuzuru ukocha PSV

Kocha wa PSV Eindhoven, Ruud van Nistelrooy ameachana na klabu hiyo kabla ya mechi ya mwisho kumaliza msimu wa ligi nchini Uholanzi.

Van Nistelrooy ameshinda kombe la ligi na Super cup ya Uholanzi baada ya kuchukua nafasi ya ukocha kwenye klabu hiyo Machi mwaka 2022.

PSV imesema kuwa mazungumzo ya kumpata kocha mwingine inaendelea baada ya kocha huyo kujiuzuru kwenye timu hiyo.

Klabu hiyo imemaliza nafasi ya pili kwenye msiamamo wa ligi kuu nchini Uholanzi ikiwa nyuma ya Feyernoord kwa jumla ya alama 10.

Klabu hiyo inatarajia kucheza na AZ Alkmaar mwisho wa wiki hii na wanakaribia kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

"Van Nistelrooy ameiambia kikosi cha kwanza benchi la ufundi kuwa anaachana na klabu hiyo haraka iwezekanavyo kutokana na kukosa sapoti ndani ya klabu hiyo”

"PSV inajutia uhamuzi wake na ina mshukuru kwa kushinda kombe la ligi na ngao ya Johan Cruijff na kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu”.

Kocha msaidizi wa PSV amechukua nafasi ya kocha wa muda wa klabu hiyo mpaka atakapopatikana kocha mweningine kabla ya kuanza kwa msimu ujao.