
Joaquin atangaza kustaafu soka
Mkongwe wa Uhispania na Real Betis, Joaquin ametangaza kustaafu soka mwisho wa msimu huu utakapoisha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 kwasasa ana misimu miwili ndani ya klabu hiyo alianza kuchezea timu ya vijana toka mwaka 2000.
Akiwa mchezaji wa Real Betis ameisaidia timu hiyo kushinda kombe la Copa del Rey mwaka 2005 kabla ya kuondoka na kujiunga na Valencia, Malaga Fiorentina na kurudi tena Valencia mwaka 2015.
"Nataka kusema kuwa muda wangu umefika” Joaquin amesema kupitia mtandao wake wa kijamii kuhusu taarifa ya kustaafu kwake.
"Muda unakuambia wewe huu ndio msimu wangu wa mwisho kama mchezaji wa Real Betis” Aliongeza mchezaji huyo
"Lakini hii sio kuagana, tutaonana hivi karibuni kwasababu nitaendelea kuwa upande wako, kutetea Maisha yangu kwasababu Real Betis imekuwa Maisha yangu” Aliendelea kusema mchezaji huyo
Mwaka jana mchezaji huyo aliiongoza Real Betis kushinda taji la pili la Copa del Rey baada ya kuwafunga Valencia kwa mikwaju ya penati.
Amecheza jumla ya mechi 521 akiwa mchezaji wa Real Betis kwa vipindi viwili tofauti ameshinda jumla ya goli 68.