21 Mar 2023 / 94 views
Evra asimulia alivyojiunga na Man United

Beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra amesema kuwa alihisi kama anafanyiwa mahojiano na Alex Ferguson wakati akimshawishi kujiunga na klabu hiyo kutokea Monaco.

Evra ameshinda mataji Matano ya ligi kuu soka nchini England, Mataji matatu ya Carabao na ligi ya mabingwa Ulaya mara moja akiwa Old Trafford.

Mchezaji huyo alikuwa amepata ofa nyingi za klabu kubwa Ulaya baada ya kufanya vizuri na Monaco ambapo hadi Liverpool walihitaji Saini yake.

Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa akaamua kujiunga na Manchester United baada ya ushawishi mkubwa sana kutoka Sir Alex Ferguson.

“Sir Alex alizungumza na wakala wangu na tukakutana katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris” Alisema mchezaji huyo

“Akuwa anaongea kifaransa vizuri pia na mimi kingereza changu hakikuwa kizuri hivyo wakala wangu alikuwa ananitafsilia” Aliongeza mchezaji huyo

“Nakumbuka alikuwa akiuliza maswali kama, ‘unakunywa?’ ‘Hapana.’ Je, unapenda kutoka nje?” “Wakati fulani.’

‘Uko tayari kutopoteza mchezo?’ ‘Ndio.’ ‘Uko tayari hata kutoteka mchezo?’ ‘Ndio’. "Ninahisi kama ilikuwa mahojiano kutoka kwa FBI.

Na nilipomshika mkono - kila ninachosema nilikuwa kama, 'niko tayari - ikiwa nitamwangusha mtu huyu ataniua', kwa hivyo ilikuwa ya kuvutia sana," aliongeza. “Kabla ya United kuja wakala wangu alisema tuna Liverpool, Inter Milan na United.