20 Mar 2023 / 105 views
PSG wapoteza mechi uwanja wa nyumbani

Klabu ya Paris St-Germain wamepoteza mechi ya nyumbani kwa mara ya kwanza toka 2021 baada ya kufungwa 2-0 dhidi ya Rennes.

Rennes wakiwa ugenini walianza kupata goli la kwanza kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Karl Toko Ekambi na kufanya 1-0 dhidi ya PSG.

Baada ya kichapo hicho PSG amepoteza rekodi yao ya kutofungwa nyumbani katika dimba la Parc des Princes ambapo walicheza mechi 35 bila kupoteza katika uwanja huo.

Reims pia ilishuhudia msururu wao wa kutoshindwa wa mechi 19 ukisimamishwa kwa kushindwa na Marseille.

Walikuwa wamepoteza mechi ya ligi mara ya mwisho mwezi Septemba kwa kufungwa 3-0 na Monaco.

Reims, inayonolewa na Mwingereza mzaliwa wa Ubelgiji, Will Still, ilichukua nafasi ya mbele kupitia kwa Folarin Balogun aliyeichezea Arsenal kwa mkopo dakika ya 13.

Lakini mabao mawili ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Alexis Sanchez yaliipa Marseille ushindi wa 2-1 huku Balogun akifunga lango katika dakika za majeruhi kipindi cha pili.

Kikosi cha Christophe Galtier cha PSG kiko pointi saba mbele ya Marseille kileleni mwa jedwali huku wakielekea kutwaa taji la 11 katika kipindi cha miaka 13.

Wakati huo huo, Rennes - ambao ni timu ya tatu tu kupata mabao mawili dhidi ya Paris St-Germain tangu Qatar Sports Investments iliponunua klabu hiyo mwaka 2011 - inashika nafasi ya tano, pointi nne dhidi ya Monaco katika nafasi ya nne na saba kutoka kwa Lens iliyo nafasi ya tatu.