
Chelsea kukutana na Madrid UEFA
Chelsea watacheza dhidi ya bingwa mtetezi Real Madrid kwenye robo fainali ya klabu bingwa Ulaya.
Mabingwa wa EPL Manchester City watacheza dhidi ya bingwa mara sita wa michuano hiyo Bayern Munich.
Inter Milan watamenyana na Benfica huku mabingwa wa Serie A, AC Milan wao watacheza na kiongozi wa Seria A, Napoli kwenye hatua yar obo fainali.
Kama Chelsea na Manchester City wanafuzu hatua hiyo watakutana kwenye hatua ya nusu fainali na watakuwa wamekutana kwenye mashindano yote msimu huu.
Michezo za mkondo wa kwanza zitacheza Aprili 11 na 12 huku mechi za marudiano zikichezwa Aprili 18 na 19 mwaka huu.
Ratiba yar obo fainali
Real Madrid v Chelsea
Inter Milan v Benfica
Manchester City v Bayern Munich
AC Milan v Napoli