18 Mar 2023 / 102 views
Bajcetic kukaa nje msimu mzima

Kiungo wa Liverpool, Stefan Bajcetic atakosa msimu wote uliobakia kutokana na kupata jeraha la nyama za paja.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amecheza mechi 19 kwa Liverpool na kushinda goli lake la kwanza dhidi ya Aston Villa Desemba mwaka jana.

Bajcetic alipata majeruhi wakati wa mazoezi na kuondolewa kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Liverpool kwenye ligi ya mabingwa ambapo walifungwa 1-0 na kuondolewa kwenye michuano hiyo.

"Ni huzuni sana kusema bai bai msimu huu uliokuwa bora kwangu’ Alisema Bajcetic

"Lakini nafahamu kuwa hii ni sehemu ya mpira na itanifanya mimi kuwa fiti kimwili na kiakili msimu ujao” Aliongeza kusema mchezaji huyo

"Pia ningependa kusema kuwa asanteni sana Liverpool wote kwa sapoti yenu kwenye msimu huu na nina uhakika nitarudi nikiwa vizuri sana”.