16 Mar 2023 / 102 views
West Ham waitamani fainali

Kocha wa West Ham United, David Moyes amesema kuwa anatamani kuona West Ham inafika fainali ya Europa Conference Ligi kueelekea mechi yao ya hatua ya 16 bora dhidi ya AEK Larnaca leo.

The Hammers walishinda 2-0 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya AEK Larnaca nchini Cyprus huku goli zote zikifungwa na Michail Antonio.defeated Larnaca 2-0

West Ham wameshinda mechi tisa katika mashindano yote hadi sasa ambapo leo wanahitaji matokeo ya suluhu tu waweze kufuzuhatua ya robo fainali.

"Kitu kikubwa tunataka kufika faina, lakini tunahitaji kufanikisha malengo yetu kwenye mashindano haya” Alisema Moyes

"Tunakazi ya kufanya kama tunataka kufanya hivyo, tushawahi kufika robo fainali kwenye mashindano mengine ya Ulaya miaka miwili iliyopita” Aliongeza Moyes

West Ham wapo kwenye nafasi mbaya ya kushuka daraja kwenye ligi kuu soka nchini England wakiwa sehemu hatari sana.