16 Mar 2023 / 91 views
Infantino achaguliwa tena

Rais wa Fifa, Gianni Infantino amechaguliwa tena kuwa rais wa Shirikisho la soka la kimataifa kwa miaka mingine minne mpaka mwaka 2027.

Infantino raia wa Uswizi na Italia mwenye umri wa miaka 52 amekuwa kiongozi mkuu wa Shirikisho la mpira la kimataifa FIFA mwaka 2016 akichukua nafasi ya Sepp Blatter.

Alishinda tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2019 ambaye alikuwa hana mpinzani kwenye kuchaguliwa kwake kwenye nafasi hiyo.

"Ni heshima kubwa sana kwangu na wajibu mkubwa sana baada ya kuchaguliwa tena nafasi hii’ Alisema Infantino kwenye mkutana wa 73 uliofanyika katika jiji la Kigali nchini Rwanda.

"Nahaidi kuendelea kulitumikia shirikisho hili kama rais wa FIFA na kuutumikia mpira duniani kote” Aliongeza kwa kusema

"Ushindi huu ni kwa wote wanaonipenda mimi na najua wapo wengi, na wote wanaonichukia mimi nawapenda wote”.