24 Nov 2022 / 68 views
De Bruyne ashangazwa kupewa tuzo

Kiungo wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne ameshangaa kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kati ya timu yake ya Ubelgiji dhidi ya Canada kutokana na kuamini kuwa hakustahili kwa sababu hakucheza vizuri.

“Sidhani kama nilicheza vizuri, sielewi ni kwanini nimepata hii tuzo, pengine ni kwa sababu ya jina langu.” Alisema De Bruyne mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mechi.

Katika pambano hilo Ubelgiji iliibuka na ushindi wa bao 1-0 bao lililofungwa na nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea na Marseille Mitchy Batshuayi.

Katika hatua nyingine Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez ambeibuka na kusema kuwa Canada ilikuwa timu bora kuliko Ubelgiji katika mchezo huo uliomalizika kwa Canada kukosa mkwaju wa penati baada mlinda mlango bora duniani kwa sasa Thibaut Courtois kupangua shuti la Alfonso Davies.