24 Nov 2022 / 63 views
Neyamar kuonyesha kiwango kombe la Dunia

Nahodha wa Brazil Thiago Silva anasema tutamwona Neymar "bora" kwenye Kombe hili la Dunia baada ya jeraha kutatiza michuano yake miwili iliyopita.

Neymar alikosa nusu-fainali ya 2014 kutokana na jeraha la mgongo, na alitatizika kujiweka sawa katika michuano ya 2018 baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu mapema mwakani.

Hata hivyo, anawasili Qatar akiwa mzima kabisa na amefunga mabao 15 katika mechi 20 akiwa na Paris St-Germain msimu huu.

"Nadhani Neymar anakuja kwenye shindano hili akiwa katika hali nzuri," alisema Silva.

“Maandalizi yake safari hii yamekuwa tofauti, mwaka 2014 aliumia kwa jinsi alivyokuwa akicheza vizuri, na mwaka 2018 aliingia kwenye michuano hiyo kwa namna tofauti kwa sababu alikuwa na majeraha makubwa hivyo alikuwa hajacheza sana. "Sasa kwa maandalizi tofauti, bila jeraha lolote na wasiwasi wowote, tunaona Neymar bora.