25 Nov 2022 / 52 views
Man United kuuzwa

Wamiliki wa klabu ya Manchester United familia ya Glazers wamekubali kuuza klabu hiyo baada ya kuimiliki Zaidi ya miaka 20.

Kupitia Statement iliyotolewa na klabu hiyo wameeleza kuwa katika mpango huo wa kuiuza timu watazingatia uwekezaji kwenye kuboresha baadhi ya maeneo ikiwemo uboreshaji wa uwanja na miundo mbinu mingine.

Inadaiwa kuwa haya yote yanakuja baada ya mahojiano ya Cristiano Ronaldo baada ya kusema kuwa wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazers hawaijali timu wanachoangalia ni pesa tu.

Klabu hiyo imekuwa chini wa familia ya Glazer kutoka Marekani kwa takribani miaka 17 na sasa wameamua kuipiga bei.