23 Nov 2022 / 73 views
Ujerumani kumenyana na Japan leo

Ujerumani lazima ijifunze kutokana na makosa yaliyopita na kuanza Kombe la Dunia la 2022 kwa nguvu, anasema kiungo wa kati Joshua Kimmich.

Wanaenda Qatar kutafuta ushindi wa kwanza wa mashindano makubwa tangu 2014 na wamepoteza mechi yao ya ufunguzi kwenye Kombe la Dunia la 2018 na Euro 2020.

Mchezo wa kwanza wa Kundi E wa Ujerumani ni dhidi ya Japan mnamo Novemba 23 huko Al Rayyan.

"Ukipoteza mchezo wa kwanza katika mashindano makubwa kuna shinikizo nyingi," Kimmich alisema katika mahojiano na Guillem Balague kwenye BBC Radio 5 Live.

Kimmich wa Bayern Munich, 27, anaonekana kwenye Kombe lake la pili la Dunia baada ya kuwa sehemu ya timu ya Ujerumani iliyomaliza mkiani mwa kundi lao nchini Urusi miaka minne iliyopita kufuatia kushindwa na Mexico katika mechi ya ufunguzi mjini Moscow.

"Bila shaka tunataka kuifanya vizuri zaidi sasa," aliongeza Kimmich. "Tulijifunza mengi, kwamba sio muhimu tu kuwa na wachezaji wakubwa, wazuri, ambao walikuwa na mafanikio mengi huko nyuma na kushinda mataji mengi.

"Inahusu kuwa na timu nzuri, tabia nzuri na ari nzuri ya timu. Lazima uwe timu bora. Huhitaji wachezaji bora ili kuwa na timu bora."

Ratiba ya kila siku na mwongozo wa TV hadi Kombe la Dunia la 2022 Jinsi ya kufuatilia Kombe la Dunia la Fifa kwenye BBC Mabingwa mara nne wa dunia Ujerumani wako katika nafasi ya 11 katika viwango vya ubora vya Fifa.

Baada ya kukabiliana na Japan, vijana wa Hansi Flick watakutana na Uhispania mnamo 27 Novemba (19:00 GMT) huko Al Khor kabla ya mchezo wao wa mwisho wa kundi dhidi ya Costa Rica mnamo 1 Desemba (19:00), pia huko Al Khor. “Bila shaka ninausubiri kwa hamu mchezo wa Uhispania,” alisema Kimmich.

"Ni mchezo wa kiwango cha juu na kila mara unataka kushindana kwa kiwango cha juu zaidi. Nadhani tunapaswa kuzingatia mchezo wa kwanza dhidi ya Japan."

Ushindi wa mwisho wa Kombe la Dunia kwa Ujerumani ulikuwa mwaka wa 2014 walipoilaza Argentina katika fainali baada ya kuwafunga wenyeji Brazil 7-1 katika nusu fainali.