10 May 2022 / 96 views
Arsenal yakaribia kufuzu ligi ya mabingwa

Klabu ya Arsenal itahitaji ushindi katika mechi ijayo dhidi ya Tottenham Hotspurs ili ikate tiketi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Arsenal imepata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Leeds United uliowafanya wafikishe alama 66 na wanahitaji kufikisha alama 69 ambazo hazitofikiwa na Spurs wenye alama 62 iwapo tu watapoteza katika dabi ya London.

Spurs ipo nafasi ya 5 kufuatia sare ya bao moja na Liverpool hivyo watahitaji kuifunga Arsenal ili kuweka hai matumaini yao kucheza UCL msimu ujao lakini pia wakiwashinikiza Chelsea ambao wana alama 67 ambao iwapo watapoteza mechi mbili za mwisho huenda wakaweka rehani nafasi yao.

Mabao ya Arsenal yaliwekwa kimiani na Eddie Nketia dakika za ya 5 na 10 huku la kufutia machozi la Leeds United likiwekwa kimiani na Diego Llorente dakika ya 66 huku wakiwa pungufu kufuatia kadi nyekundu ya Luke Ayling aliyoonyeshwa dakika ya 27 ya mchezo.

Nayo Everton inayonolewa na Kocha Frank Lampard, imechomoka kwenye mstari wa timu tatu zitakazoshuka daraja kufuatia ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Leicester City na sasa wamefikisha alama 35 wakiwa nafasi ya 16 wakiziacha Burnley katika nafasi ya 17 na alama zao 34 nayo Leeds United yenye alama 34 wakiwa katika nafasi ya 18.