06 Apr 2022 / 381 views
Chama mchezaji bora NBC

Kiungo wa Simba, Clatous Chama ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa tatu wa ligi kuu ya NBC na kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Simba kutwaa tuzo hiyo.

Chama anakuwa mchezaji wa saba kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika ligi kuu huku kwa mwezi March akiwabwaga nyota wawili Fiston Mayele (Yanga) na Frank Kahola (Mtibwa Sugar ) waliongia kwenye kinyang'anyiro cha mwezi huo.

Na kocha mkuu wa klabu ya Simba, Pablo Franco ambaye ni mara ya kwanza na yeye kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi March wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC Premier league) 2021/22 baada ya kuwa na matokeo bora kwa mwezi huo .

Pablo aliiongoza Simba kupata matokeo ya ushindi kwenye michezo miwili dhidi ya Biashara Mara United na dhidi ya Dodoma Jiji.

Pablo amewashinda makocha wawili Nasreddine Nabi (Yanga Sc) na Francis Baraza ( Kagera Sugar) walioingia kwenye fainali ya mwezi March ihali tuzo ya meneja bora wa uwanja imekwenda kwa meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa ,Nsajigwa Gordon kwa kufanya vizuri kwenye michezo iliyofanyika kwenye uwanja huo kwa mwezi march na kulinda miundombinu ya uwanja kwa ujumla.