08 Mar 2022 / 97 views
Mkataba wa Lewandolski wakaribia kumalizika

Bayern Munich wanaweza kufanya vyema zaidi kuangazia mechi yao ya katikati ya juma la hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa, lakini huku Robert Lewandowski akiwa na shauku ya kutaka kusaini mkataba mpya, uvumi wa uhamisho kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo wa Poland unazuia suala hilo.

Bayern wanawakaribisha Red Bull Salzburg katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne kufuatia sare ya 1-1 huko Austria.

Katika hali isiyo ya kawaida kwake, Lewandowski hajafunga bao katika mechi zake tatu zilizopita na nje ya uwanja, mustakabali wake zaidi ya msimu huu haueleweki.

Mwishoni mwa wiki, kulikuwa na ripoti kwamba Manchester United inaongoza orodha ya vilabu vya Premier League kuwasiliana na wakala wa Lewandowski Pini Zahavi.

Lewandowski, 33, kama maveterani wenzake wa Bayern Manuel Neuer, 35, na Thomas Mueller, 32, mkataba wake unamalizika Juni 2023.

Ingawa Neuer na Mueller wameripotiwa kuambiwa ana kwa ana kwamba klabu inataka kuongeza muda, Lewandowski hajafanya hivyo.

Mwezi uliopita, mkurugenzi wa Bayern Hasan Salihamidzic alisema hadharani kwamba klabu haitaki kumuuza. "Ni nje ya swali. Robert ni sehemu muhimu sana ya timu".