
Aubameyang aanza mazoezi
Mshambulizi wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang amerejea mazoezini na kikosi cha Gabon kabla ya mechi ya Ijumaa ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Ghana baada ya kukutwa hana Covid-19.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye hapendelewi na Arsenal na alinyang'anywa unahodha mwezi uliopita na Mario Lemina wote walipatikana na virusi wiki iliyopita na wakakosa ushindi wa kwanza wa Gabon wa 1-0 dhidi ya Comoro Jumatatu.
Hata hivyo, kocha Patrice Neveu anajitenga baada ya kukutwa na virusi hivyo kulingana na shirikisho la soka la Gabon.
Gabon imekuwa na hali ngumu katika maandalizi ya mashindano ya mabara yanayofanyika kila baada ya miaka miwili.
Serikali ya Gabon ililazimika kusuluhisha mzozo kati ya wachezaji na shirikisho kuhusu bonasi za mechi huku Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likiwasuta kwa kuvunja sheria za kubadilisha hoteli mjini Yaounde.