Sababu ya Carrick kumuacha Ronaldo nje
Kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick amesema ulikuwa uamuzi wake kumuacha nje Cristiano Ronaldo katika mchezo dhidi ya Chelsea.
Beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville alisema kuwa kabla ya mchezo kuwa Mjerumani Rangnick alikuwa amechagua timu kwa ajili ya mechi lakini Carrick alipuuza maoni ya mchambuzi.
"Nilijua jinsi Chelsea wangecheza na tulitaka kuzima pasi za Jorginho na Ruben Loftus-Cheek. Kulikuwa na mabadiliko machache ya kuiboresha na ndiyo tuliamua kwenda nayo. Karibu tuvute."
Ronaldo, ambaye alianza na kufunga katika ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki dhidi ya Villarreal, aliingia dakika ya 64 dhidi ya Chelsea.
Jadon Sancho aliifungia United bao la kuongoza lakini Chelsea walisawazisha kupitia kwa mkwaju wa penalti wa Jorginho.
Manchester United, ambayo iko katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, pointi 12 nyuma ya vinara Chelsea, itaikaribisha Arsenal siku ya Alhamisi.