19 Nov 2021 / 100 views
Tetesi za usajili Ulaya

Manchester United na Chelsea wamepata nguvu katika harakati zao za kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, ambaye kipengele chake cha kuachiliwa kinamwezesha kuondoka kwa pauni milioni 64 msimu ujao, huku Real Madrid wakikubali mshambuliaji huyo wa Norway, 21, kuhamia ligi ya Primia.

Real wanapanga kushindana na Chelsea, Manchester City na Paris St-Germain kwa kumuongeza mshambuliaji wa Haaland na mshambuliaji wa PSG Mfaransa Kylian Mbappe, 22, kwenye safu ya ushambuliaji ambayo tayari inamshirikisha Mbrazil Vinicius Junior, 21.

Newcastle United wanapanga kumsajili mlinzi wa Uholanzi Stefan de Vrij, 29, na kiungo wa kati wa Croatia Marcelo Brozovic, 28, kutoka Inter Milan mwezi Januari, pamoja na kipa wa Lazio wa Albania Thomas Strakosha, 26.

Wakala wa Paul Pogba amedokeza kuwa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 28, ataondoka Manchester United mwezi Januari, kabla ya mkataba wake kumalizika msimu wa joto.

Manchester United wanatazamiwa kushindana na Barcelona katika kutaka kumsajili winga wa RB Leipzig wa Kihispania Dani Olmo, 23. 

Chelsea wanavutiwa na mlinzi wa Leicester City Wesley Fofana na wako mbele kidogo ya Manchester United katika kujaribu kumsajili beki huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20.

Barcelona wanapanga kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Hakim Ziyech lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Borussia Dortmund kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco, 28.

Mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, amekasirishwa na ofa ya hivi punde ya Chelsea ya kandarasi, ambayo ni pungufu ya mahitaji yake ya mshahara ya pauni 60,000 kwa wiki.

Arsenal wako tayari kumpa mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette mkataba wa muda mfupi huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akikaribia mwisho wa mkataba wake msimu ujao wa joto.