
Benzema hatoachwa timu ya taifa
Mshambulizi wa Ufaransa Karim Benzema "hatatengwa" katika uteuzi wa timu ya taifa ikiwa hukumu ya hatia itatolewa dhidi yake katika kesi inayoendelea ya kanda ya ngono, kulingana na rais wa shirikisho la soka la Ufaransa Noel Le Graet.
Katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la kila siku la Ufaransa Le Parisien, Le Graet alisema uamuzi wowote kuhusu nani atachaguliwa kwa majukumu ya kitaifa utabaki kuwa uamuzi wa kocha Didier Deschamps.
Benzema aliondolewa kwenye kikosi cha Ufaransa kwa miaka mitano hadi alipoitwa tena mwezi Mei mwaka jana baada ya kushutumiwa kuhusika katika udukuzi wa mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena kuhusu kanda ya ngono.
"Kocha atakuwa ndiye mtu anayechagua upande na Benzema hatatengwa katika kesi ya hukumu ya hatia," Le Great alisema.
Benzema anatarajiwa kupangwa wakati mabingwa watetezi wa dunia Ufaransa watakapomenyana na Kazakhstan mjini Paris siku ya Jumamosi katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022.
Upande wa mashtaka ulitaka Benzema apewe adhabu ya kusitishwa kwa miezi 10, ambaye mawakili wake wamedai kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kumtia hatiani nyota huyo kwa kuhusika na ubadhirifu.