14 Jul 2021 / 130 views
Tetesi za usajili Ulaya

Kocha wa Liverpool Jurgen kuhitaji kuboresha zaidi safu ya ushambuliaji ya kikosi chake, lakini PSG wanamuhitaji Pogba.

Klabu ya Chelsea ya England ipo tayari kulipa ada ya uhamisho ya pauni million 150, zaidi ya bilioni 476 kwa pesa za kitanzania kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Norway na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujermani Erling Haaland mwenye umri wa miaka 20, inaaminika kuwa endapo Chelsea watalipa dau hilo Dortmund hawatakataa ofa hiyo. Vilabu vingine vinavyomuwania mshambuliaji huyo ni Real Madrid na Fc Barcelona vya Hisapania, na Manchester City ya England.

Tottenham, Leeds United, na Manchester City zinapigana vikumbo kumuwania winga wa Sampdoria ya Italia na timu ya taifa ya Denmark Mikkel Damsgaard mwenye umri wa miaka 21. Wakala wa mchezaji huyo amefanya mazungumzo na vilabu kadhaa vya England baada ya mchezaji huyo kuonyesha kiwango bora kwenye michuano ya Euro 2020 na Rais wa klabu ya Sampdoria Massimo Ferrero amesema thamani ya mchezaji huyo imepanda kutokana na kiwango chake kwenye michuano ya Euro.

PSG ipo tayari kulipa Euro million 50 mpaka 60 ambayo si chini ya Bilion 137 mpaka bilioni 164 kwa pesa za Tanznaia kama pesa ya ada ya uhamisho ya kumsajili kiungo wa Manchester United Paul Pogba ambaye mkataba wake na Man United unamalizika mwishoni mwa msimu ujao wa 2021-22. Inaripotiwa kuwa Pogba hajafanya mazungmzo ya mkataba mpya na The Red Devils na inatajwa kuwa yupo tayari kujiunga na PSG.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa anahitaji kusajili wachezaji watatu kwenye kikosi chake ili kurejesha makali na kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa EPL msimu ujao, miongoni mwa wachezaji wanao tajwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji aliopendekeza Kocha Klopp ni Youri Tielemans wa Leicester City, Kiungo wa Lille ya Ufaransa Renato Sanches na winga wa Bayern Munich Kingsley Coman.