
Ratiba ya UEFA leo
Kwenye Ligi ya Mabingwa, Real Madrid kuwaalika Atalanta leo usiku pale Alfredo Di Stefano. Je, faida ya goli 1 la ugenini itawavusha Madrid au Atalanta watapindua meza.
Klabu ya Manchester City leo itawakaribisha Borussia Monchenglabach kwenye mechi ya pili ya ligi ya mabingwa katika uwanja wa Etihad.
Chelsea atakuwa Stamford Bridge kuwaalika Atletico Madrid. Kama ilivyo kwa Madrid, Chelsea anafaida ya goli 1la ugenini.
Kunako Ligi ya Europa alhamisi hii ni Dynamo Zagreb vs Tottenham Hotspurs kwenye mechi ya pili baada ya kushinda mechi iliyopita.
Baada ya sare ya 1-1 pale Old Trafford, Manchester United dhidi ya AC Milan sasa vita inahamia Italia, nani atasonga mbele msimu huu.