14 Dec 2020 / 348 views
Ratiba ya Uefa champions league

Manchester City watamenyana na Borussia Monchengladbach, ambao wako kwenye 16 bora kwa mara ya kwanza tangu 1978.

Bayern Munich watakutana na Lazio ya Italia, ambao wako kwenye hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika miaka 20.

Barcelona inakabiliwa na Paris St-Germain toka walipokutana mara ya mwisho mwaka 2017 katika michuano hiyo ya Ulaya.

Timu zote tatu za Uingereza zitakuwa ugenini kwa mchezo wao kwanza kabla ya kuwa na faida ya nyumbani kwa mechi za marudiano.

Mzunguko wa kwanza itafanyika katikati ya wiki mbili, ikifanyika tarehe 16, 17, 23 na 24 Februari, na raundi ya pili tarehe 9, 10, 16 na 17 Machi.

Ratiba kamili

Borussia Monchengladbach v Manchester City

Lazio v Bayern Munich

Atletico Madrid v Chelsea

RB Leipzig v Liverpool

Porto v Juventus

Barcelona v Paris St-Germain

Sevilla v Borussia Dortmund

Atalanta v Real Madrid