
Neymar kucheza na Messi timu moja
Neymar aliwashangaza wengi aliposema kwamba anataka kucheza na Messi tena msimu ujao , muda mfupi baada ya kuisadia PSG kupata ushindi wa 3-1 katika mashindano ya kombe la klabu bingwa Ulaya dhidi ya Man United.
''Kile ninachohitaji sana ni kucheza tena na Linel Messi , ili kuweza kumfurahikia tena uwanjani'', Neymar aliambia chombo cha habari cha ESPN kuhusu mchezaji mwenza wa Barcelona.
''Anaweza kucheza katika nafasi yangu , sina wasiwasi na hilo. Lakini nataka kuungana naye mwaka ujao kwa kweli. Lazima tuhakikishe kwamba hilo linafanyika mwaka ujao''.
Ufichuzi huo unajiri huku kaimu rais wa klabu hiyo Carlos Tusquets akisema kwamba klabu hiyo ingemuuza Messi msimu uliopita.
Mshambuliaji wa Argentina Messi mwenye umri wa miaka 33 aliambia Barcelona kwamba alitaka kuondoka wakati huo na kusema kwamba kifungu kimoja katika kandarasi kilimaanisha kwamba angeweza kufanya hivyo akiwa huru.
Barca ilisema kwamba hilo halikuwa lengo lao na kwamba hawatamruhusu mfungaji wao wa magoli mengi na nahodha kuondoka kwa chini ya £624m.
Josep Maria Bartomeu alijiuzulu kama rais wa klabu hiyo mnamo mwezi Oktoba huku Tusquest akichukua uongozi kwa muda hadi uchaguzi utakapofanyika mwezi Januari.
Zote kwa mujibu ya utakachohifadhi katika mshahara pamoja na fedha zinazoingia , ingekuwa bora.
Kandarasi ya Messi inakamilika msimu ujao na mwandishi wa kandanda wa Uhispania Guillem Balague, akizungumza na BBC anasema kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo.