Simba yafanya usajili mpya
Kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda Taddeo Lwanga amesaini dili la miaka miwili kuitumia Klabu ya Simba na leo Desemba 2 ametambulishwa rasmi.
Nyota huyo amewahi kuzichezea timu za Express FC, SCV Kampala, Vipers FC na Tanta FC hivyo uzoefu wake na uwezo wake ndani ya uwanja ni sababu ya kupewa dili ndani ya Simba.
Nyota huyo alikuwa kwenye rada za mabosi hao kwa muda mrefu baada ya kiungo wao Gerson Fraga raia wa Brazil kupata majeraha ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Fraga aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United na nafasi yake ilichukuliwa na Said Ndemla.
Usajili wa Lwanga unatokana na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kutoa nafasi za wawakilishi wa mashindano ya kimataifa kusajili wachezaji 10 ili kuongeza nguvu katika mashindano hayo.