04 Nov 2020 / 183 views
Matokeo ya mechi za UEFA

Mechi za hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu 2020/21 zimeendelea kuchezwa kwenye viwanja mbalimbali. Jana Novemba 3 2020, zilichezwa jumla ya mechi nane na kushuhudia vipigo vizito.

Ni mechi  tatu pekee ndizo zimemalizika kwa ushindi wa magoli mengi ambapo ni mechi ya Shakhtar wakiwa nyumbani wamefungwa 0-6 na Mönchengladbach, RB Salzburg wakiwa nyumbani kwao wamefungwa 2-6 na Bayern Munich huku Liverpool nao wakiwa ugenini wameichapa Atalanta 5-0.

Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa anaona vijana wake wanafanya yale ambayo mashabiki wanahitaji pamoja na kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

"Ninaona vijana wangu wanafanya kile ambacho tunahitaji kupata ndani ya uwanja ambacho ni ushindi, hata mashabiki pia wanahitaji kuona timu inashinda.

"Bado kazi ipo na tuna jukumu la kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo, uwezo upo na sapoti ni kubwa," amesema.