
Tetesi za usajili barani Ulaya
Kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil Arthur, 23, anakaribia kukubali uhamisho wa kima cha euro 72.5 milioni kuelekea Juventus, huku kiungo wa kati wa Bosnia Miralem Pjanic, 30, akipigiwa upatu kujiunga na upande mwingine kwa £54.25m.
Winga wa Uhispania Pedro, 32, atajiunga na Roma kwa mkataba wa miaka miwili mkataba wake Chelsea umwisho wa msimu huu.
Bayern Munich haitajiunga na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wakati wa Birmingham wa miaka 16-Jude Bellingham, ambaye pia ananyatiwa na Borussia Dortmund.
Arsenal walikuwa tayari kumlipa mshambuliaji wa Chelsea Mbrazil Willian, 31, euro 250,000 elfu kwa wiki kabla ya kuibuka kwa janga la corona.
Leeds United wanakaribi akumsajili kiungo wa kati wa England Jadan Raymond, 16, baada ya kinda huyo kukataa mkataba wa kwanza wa kitaalamu Crystal Palace.
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amemwambia mwenyekiti wa Daniel Levy kwamba anataka kuwasajili wachezaji watano wampya msimu huu wa jotoi lakini Spurs wanalenga zaidi mikataba ya mkopo na kuwasajili wachezaji ambao mikataba yao imekamilika.
Kocha Brendan Rodgers amemwambia James Maddison kwamba Leicester ndio 'mahali pazuri' kwake baada ya kiungo huyo wa England, wa mika 23, kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Manchester United.
Winga wa Real Madrid naColombia James Rodriguez, 28, ambaye amesalia na mkataba wa mwaka mmoja, bado ana tafakari uwezekano wa kujiunga na Napoli.
Arsenal na AC Milan wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Red Bull Salzburg kumhusu kiungo wa kati wa Hungary Dominik Szoboszlai, kuhu Paris St-Germain wakisemekana pia wakimuulizia kiungo huyo wa miaka 19.